• Fri. Oct 30th, 2020

Wanaharakati watano wameenda mahakamani  kuzuia katiba kufanyiwa marekebisho kupitia juhudi zinazoendelea za Jopo La Maridhiano (BBI).Wanaitaka Mahakama kuu itangaze kwamba Sura ya Tisa ya Katiba inayohusu Serikali Kuu, haiwezi kurekebishwa na Bunge wala kupitia kauli ya wananchi kwenye kura ya Maamuzi.

Sura nyingine wanazotaka zichukuliwe kuwa ‘zisizoweza kurekebishwa’ ni ile ya kwanza inayohusu Nguvu ya Wananchi na Utukufu wa Katiba, Sura ya pili kuhusu Jamhuri,Sura ya nne inayohusu Haki mbalimbali na Sura ya Kumi Inayozungumza kuhusu Idara ya Mahakama. Wanaitaka mahakama kutangaza kuwa sura hizo tano za Katiba zisiguzwe na yeyote.

Wakiongozwa na  Bw David Ndii, wanaharakati Jerotich Seii, James Ngondi, Wanjiku Gikonyo na Ikal Angelei, wanataka mahakama ieleze wanaonuia kuleta mabadiliko kwamba ni vipenge vichache mno vinavyoweza kurekebishwa. Iwapo mahakama itakubali maombi yao, uamuzi utaathiri juhudi zinazoendelezwa za kubadili katiba maarufu kama ‘reggae’.

Follow us in social media:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *