• Sat. Oct 31st, 2020

Mchunga kondoo awa kinyonga

Byjess

Aug 6, 2020 ,

Sheikh mmoja Kaunti ya Mombasa akamatwa  Jumanne usiku kwa kosa la kumuoa na kumpachika mimba msichana mwenye umri mdogo aliyekuwa katika kituo cha watoto kinachomilikiwa na Shekhe huyu.Ustadh Salim Dzomba Omar mwenye umri wa miaka 42,anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Bamburi  huku uchunguzi ukiendelea.

Kituo cha Markaz Answar kilicho Mwakirunge kilikuwa na watoto 36 waliotoka Kaunti ya Kilifi,Mombasa na Tana River.Kulingana na OCPD wa Kisauni Justin Kiragu, watoto hao wamechukuliwa na kupelekwa  vituo vilivyo salama na walio na makwao wanasubiri kupelekwa nyumbani.“Ustadh huyo alimchukua na kumuoa msichana aliyekuwa chini ya ulinzi wake katika kituo hicho na kwa sasa  binti huyo ana mimba iliyo na miezi minne.Uchunguzi unaendelea ili tuweze kubaini umri wa msichana huyu ili mshukiwa aweze kufikishwa mahakamani,”Bwana Kiragu akasema.

Kulingana na Dini la Kiislamu iwapo  ushahidi waonyesha Shehe huyu alifanya tendo hilo angehukumiwa kwa kupigwa mawe ila humu Nchini Kenya lazima haki ifuatwe kupitia korti.Uamuzi wa mahakama utatekelezwa pindi shahidi atakapotoa ushahidi wa kutosha.Hili ni jambo la kusikitisha na lililo na aibu kumwona mtu anayepewa heshima na mamlaka na jamii na Dini kukosa maadili kwa kufanya tendo hilo.Licha ya kujishusha dhamana ametia dosari kwenye maisha ya msichana huyo na kumwacha na donda sugu la kuwa mmoja wa waathiriwa wa mimba za mapema.

Follow us in social media:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

COVID-19 Pandemic Updates

The outbreak of coronavirus disease (COVID-19) has been declared a pandemic and the virus has now spread to many countries and territories. While a lot is still unknown about the virus that causes COVID-19, we do know that it is transmitted through direct contact with respiratory droplets of an infected person (generated through coughing and sneezing) Individuals can also be infected from touching surfaces contaminated with the virus and touching their face (e.g., eyes, nose, mouth). While COVID-19 continues to spread it is important that communities take action to prevent further transmission, reduce the impacts of the outbreak and support control measures.