• Sun. Aug 9th, 2020

Naibu Rais Awataka Maseneta Kuandaa Mfumo Bora Wa Ugawi Wa Fedha

Byjess

Aug 1, 2020 ,
NAIBU RAIS WILLIAM RUTO

NAIBU Rais William Ruto awasihi maseneta kuandaa mfumo wa ugawi wa fedha kwa kaunti utakao hakikisha kuwa kaunti zoye 47 zinafaidi. Kulingana naye Serikali ya Kenya ni serikali ya walio wengi na walio wachache. Wananchi wote walioko pembe zote za nchi na waliotengwa miaka ya nyuma kwa hivyo maseneta wanapojadiliana kuhusu mfumo wa ugawi wa fedha walenge kuunganisha taifa .

Dkt Ruto alisema,” mfumo ambao wote wanaibuka washindi unaweza kupatikana .Lakini ule ambao utawaacha wengine wakihisi kupoteza ili wengine wafaidi utaishia kuligawanya taifa.”Jumanne wiki jana,mfumo ambao unaupa uzito idadi ya watu ulikataliwa na maseneta wengi licha ya kiranja wa wengi Irungu Kang’ata kupendekeza uanze kutumika baada ya miaka miwili ,yaani katika mwaka wa kifedha wa 2022/2023.

William Ruto alisema haya akiwa eneo-bunge la Aldai, Kaunti ya Nandi alikohudhuria hafla ya mazishi ya Mama Hellen Serem, mamake mbunge wa eneo hilo Cornelly Serem.

Follow us in social media:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

COVID-19 Pandemic Updates

The outbreak of coronavirus disease (COVID-19) has been declared a pandemic and the virus has now spread to many countries and territories. While a lot is still unknown about the virus that causes COVID-19, we do know that it is transmitted through direct contact with respiratory droplets of an infected person (generated through coughing and sneezing) Individuals can also be infected from touching surfaces contaminated with the virus and touching their face (e.g., eyes, nose, mouth). While COVID-19 continues to spread it is important that communities take action to prevent further transmission, reduce the impacts of the outbreak and support control measures.