• Sat. Oct 24th, 2020

Sheria mpya kufinya KTDA

Byflorence wairimu

Aug 4, 2020

Mapato ya Shirika la Majani Chai[KTDA] yanatarajiwa kupungua kwa kiasi kikumbwa kuanzia Novemba mwaka huu.Sheria za Chai za 2020 zimepunguza kiasi cha ada ya usimamizi ambayo KTDA imekuwa ikiwatoza wakulima kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 1.5 ya mapato yao.Waziri wa Kilimo Peter Munya alisema kuwa KTDA itafuata sheria hiyo mpya kikamilifu.

Waziri alikuwa akizungumza alipotoa mwongozo kuhusu namna kanuni zinazolenga kulainisha sekta ya majani chai zitakavyotekelezwa.

‘Ada ya kila mwaka haistahili kuzidi asilimia 1.5 ya mapato ya chai yaliyouzwa mnadani,’Waziri Munya alisema .Wakurugenzi wa KTDA wanaofanya biashara na viwanda vya chai vilivyo chini ya shirika hilo wafaa kujiuzulu nyadhifa kufikia Februari mwaka ujao mwaka ujao.Hatua hii inalenga kuzima upendeleo katika maamuzi.

Kulingana na kanuni mpya, KTDA itawalipa wafanyikazi wake wanaohudumu katika viwanda.Hii ni tofauti na hapo awali ambapo viwanda vililazimika kulipa wafanyikazi wanaoletwa na KTDA.Wizara ya kilimo pia imepiga marufuku mauzo ya majani chai katika soko la kimataifa bila kupitia mnada wa Mombasa.Pia imepigwa marufuku kuuza majani chai nje ya nchi kupitia tawi tawi lake la Chai Trading.Madalali,wauzaji na waandalizi wa minada ya majani chai watapeleka fedha za mapato kwenye akaunti za viwanda husika katika muda wa siku 14 baada ya mauzo.

Follow us in social media:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *