• Fri. Oct 30th, 2020

Tulisahaulika-Kapetadie

Byjess

Aug 20, 2020 ,

Kapetadie ni eneo lilipo  mpaka wa Kenya na Sudan Kusini kwenye jimbo la Turkana Magharibi.Kata ya Turkana imepewa sifa tangu Gavana alipotangaza wataanza kuchimba mafuta lakini licha ya utajari huu maeneo mengi huku yana shida sana.Watu wengi huku hufa kwa njaa,wengine vita na hili husababisha maafa mengi mno.Eneo la Kapetadie lipo Kilomita 50  Kaskazini mwa mji wa Lokichogio ila ni kama limesahaulika na Serikali ya Kenya.

Licha ya eneo hili kuwa kwenye ramani ya Kenya,watu wa Kapetadie wakitaka huduma za Serikali wao huenda mji wa Looiding au Lokichogio na ni safari ya Kilomita 50.Tatizo hili huwaacha mikononi mwa Wanamgambo wa Sudan Kusini ambao ni wa Jamii la Kikabila la Wanatoposa.

Taasisi ya kujifunza huku Kapetadie ni shule moja tu ya Chekechea na hivyo basi baada ya mwaka mmoja wa masomo watoto wengi husitisha masomo yao hapo na kuingilia ufugaji wa mifugo.Kulingana na bwana Emanikor Lokadeli ambaye ni mfugaji,wao hutegemea neema za Mwenyezi Mungu kwani hawana huduma muhimu,hakuna mtu ambaye hutaka kuwekeza kwenye eneo lao na ata haoni kama wao huhesabiwa kama wananchi wa Kenya. ‘’Sisi huenda miguu mpaka jimbo la Lokichogio ili kutafuta chakula na kupata dawa ugonjwa ukisidizi.Sisi tushajifunza kutumia dawa ya jadi kwani huduma za hospitali zipo mbali sana,’’bwana Lokadeli alisema.

Ombi kuu la watu wa eneo hili ni serikali iwakumbuke na iwasaidie kwani changamoto wanazozikumba ni tele mno.Wakaazi wa Kapetadie wana hofu kuwa Wanamgambo wa Toposa wanaeza waeka mateka milele pindi tu watakapochukua uongozi wote wa eneo hili.Wakaazi hawa wamechoka kukandamizwa wakiwa kwao na hata wengine wao kuuliwa bila sababu yoyote.Ukosefu wa usalama ni tatizo lao kuu.

Follow us in social media:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *